
Katika taarifa yake, Kocha wa timu hiyo, Hassan Banyai amesema, yupo katika mawindo kutafuta wachezaji wa maana nje ya nchi ambao watakuja kuibeba timu hiyo kwenya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao.
Banyai amesema, mbali na Uganda, wametuma maskauti nchini Congo pamoja na Nigeria kusaka vijana wenye uwezo ili kukitumikia kikosi hicho.
Majimaji iliyorejea ligi kuu uliopita mpaka sasa imefanikiwa kunasa saini ya kipa wa Mbeya City David Burhan pamoja na beki wa kulia villa Squard Godfrey Taita ambaye ni mzoefu wa ligi kuu.