Tuesday , 5th Jan , 2016

Mashabiki 6000 wa Real Madrid wamejitokeza asubuhi ya leo kumwamgalia kocha mpya wa muda wa Real Madrid Zinedine Zidane akielekeza mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Valdebebas,mjini Madrid.

Zidane akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Real Madrid mapema leo asubuhi,huku nyuma maelfu ya mashabiki wakishuhudia

Mashabiki 6000 wa Real Madrid wamejitokeza asubuhi ya leo kumwamgalia kocha mpya wa muda wa Real Madrid Zinedine Zidane akielekeza mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Valdebebas,mjini Madrid.

Zidane mwenye umri wa miaka 43,mchezaji wa zamani wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ufaransa,ameteuliwa jana jioni kuchukua mikoba ya kocha aliyetimuliwa Rafael Benitez.

Zidane ataanza kibarua chake cha kwanza kwenye klabu hiyo kwenye mechi dhidi ya Deportivo La Coruna jumamosi wiki hii.
Zidane aliyekuwa msaidizi wa Benitez,amesema"hii ni siku muhimu kwangu.nimesisimka sana hii leo,kuliko siku ambayo nilisajiliwa kama mchezaji.Nitafanya kazi kwa bidii na wachezaji wote,na nadhani itakuwa vizuri".

Zidane alishinda ubingwa wa La Liga mara moja 2003 na ubingwa wa Ulaya mara moja mwaka 2002 akiwa Real Madrid kama mchezaji,pia alitwaa kombe la dunia na timu ya taifa ya Ufaransa,na hadi anateuliwa kuchukua nafasi ya ukocha hapo jana,alikuwa kocha wa kikosi B cha Real.

Real Madrid imevunja mkataba na Benitez baada ya mwendo wa kusuasua kwa klabu hiyo ambayo hadi sasa inashikilia nafasi ya tatu ya msimamo wa La Liga,ikiwa pungufu ya pointi nne na vinara wa ligi hiyo Atletico Madrid na pointi mbili pungufu na anayeshika nafasi ya pili Barcelona.