Wednesday , 3rd Jul , 2019

Kuelekea msimu wa 2019/20 wa Ligi kuu soka nchini England, chama cha soka (FA), kimeweka wazi baadhi ya mabadiliko ya kanuni katika msimu huo.

Manchester City walipochukua ubingwa

Mabadiliko hayo yanahusisha kuanza kutumika kwa teknolojia ya Video (VAR), pamoja na maeneo itakayotumika.

1. Mipira iliyosimama (Drop Ball)
Endapo mwamuzi atasimamisha mpira kwa dharura yoyote, timu iliyokuwa ikimiliki mpira huo itapewa kuanzisha na itaamua kama itautoa nje ili wapinzani warushe au iendelee kucheza tu.

2. Mipira ya kuguswa na mkono (Hand Ball)
Mpira wowote utakaoingia golini huku ukiwa umeguswa kwa mkono na mfungaji hata kama kwa bahati mbaya au kwa kudhamiria hautahesabika kama goli.

3. Ukuta kwenye mipira ya dhabu (Wall)
Hapa washambuliaji wa timu pinzani wamezuiwa kushiriki kwenye ukuta na badala yake wanatakiwa kuwa mita 1 kutoka eneo la ukuta.

4. Matumizi ya Teknolojia ya video (VAR)
Msimu huu Premier League itaanza kutumia VAR rasmi lakini kanuni zake zimeanisha wazi kuwa teknolojia hiyo itatumika tu kwenye matukio ya utata kama goli na kadi nyekundu.