Thursday , 7th Jan , 2016

Katika kuhakikisha JKT Ruvu haishuki daraja, kocha wa kikosi hicho, Abdallah King Kibadeni, amesema hana masihara na ameamua kuendeleza mazoezi kipindi hiki cha likizo fupi ya wiki mbili.

JKT ambayo ilisimika mizizi mkiani mwa msimamo kwa muda mrefu tangu kuanza kwa ligi, kwa sasa ipo nafasi ya 10 na pointi 12, hata hivyo, King Kibadeni amesema bado hawajajihakikishia kukwepa mstari wa kushuka daraja, ndiyo maana ameamua kuendeleza program za mazoezi.

Kocha huyo mkongwe amesema ameamua kuweka kambi Chanika kutokana na utulivu wa mazingira.

Kibaden amesaema bado hawako salama katika janga la kushuka daraja ndio maana ameona kuna kila sababu ya kuendelea na programu za mazoezi.