Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema, kambi hawajaanza rasmi lakini wanaendelea na mazoezi ya wachezaji walionao ambao bado hawajaanza kambi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Hafidh amesema, wanatarajia kuanza kambi rasmi na wachezaji wote Septemba saba wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi ambayo inaanza Septemba 12 na wanaamini kambi hiyo itakuwa na nguvu kwani kikosi walichonacho kinaendelea na mazoezi na wale walio timu ya taifa wanaendelea na mazoezi katika kambi hiyo.
