Tuesday , 25th Mar , 2014

Mabondia watanzania Tomas Mashali na Japhet kaseba wako katika maandalizi ya mwisho mwisho wakijiwinda na mpambano wao wa kimataifa kuwania ubingwa wa UBO utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaam

Rais wa TPBO Yasin Abdalah ustaadh akiongea kwaniaba ya wasimamizi wa pambano hilo PST amesema kimsingi maandalizi yote yamekamilika kwa kiasi kikubwa huku baadhi ya mabondia wa utangulizi toka mkoani Tanga nao wakiwasili jijini Dae es salaam hapo kesho

Huku pia Ustadh akiwataka mabondia wote kufika kwa wakati hasa siku ya ijumaa siku ambayo kutafanyika zoezi la mwisho kabisa la upimaji uzito kwa mabondia wote watakaovaana siku ya jumamosi march 29 katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.