Kikosi cha wanapaluhengo kwenye piacha ya pamoja katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora mkoani Iringa
Katibu mkuu wa klabu hiyo Wille Chikweo amesema kuwa kwa sasa timu yao inaendelea kufanya mazoezi kabambe kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam na wana uhakika watakaporejea kwenye mshikemshike wa ligi hiyo wataonesha kile walichodhamiria.
Chikweo ametamba kuwa uwepo wa nyota kama Dany Mrwanda, Yona Ndabila, Salum Machaku na Nurdin Bakari kumewaongezea uzoefu nyota wengine wanaochipukia hivyo wana imani watatamba msimu huu kwenye ligi daraja la kwanza.
Lipuli ambayo ilitamba miaka ya 2000 inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B kwenye ligi hiyo ikiwa imejivunia alama 10 huku kinara wa kundi hilo Ruvu Shooting ikiwa na alama 16.


