
Jesse Lingard (Kushoto) na Maecus Rashford
Lingard, aliwahi kuitwa mara moja kipindi cha nyuma, lakini hakutumika kwenye mchezo wa England wa ushindi wa mabao, 2-0 dhidi ya Ufaransa katika mwezi wa Novemba mwaka uliopita.
Mchezaji mwingine wa United, Marcus Rashford, ameitwa tena kwenye kikosi hicho cha wakubwa, baada ya kuonesha kiwango kizuri alipoifungia hat-trick, timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, dhidi ya Norway mwezi uliopita.
Naye, mlinzi wa Stoke City, Glen Johnson ameitwa tena kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014, huku winga wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain naye akirejea baada ya kukaa benchi kwa muda mrefu.