
Kikosi cha Vijana cha Simba SC (Picha: Maktaba)
Tayari klabu hizo zimepewa shilingi milioni 10 (Sh 10,000,000) kutokana na udhamini wa ligi hiyo, huku pia zikitarajiwa kuongezewa shilingi milioni 10 (Sh 10,000,000) nyingine kutokana na udhamini mwingine wa Matangazo.
Vituo vilivyopangwa ni Dar es Salaam ambako kuna timu za JKT Ruvu, Simba, Ruvu Shooting, Ndanda, Majimaji ya Songea, Mtibwa, Mbeya City na Tanzania Prisons.
Kituo kingine ni Bukoba mkoani Kagera ambako kuna timu za Azam, African Lyon, Mbao FC, Toto Africans, Mwadui ya Shinyanga kama ilivyo Stand United, Kagera Sugar na Young Africans ambazo zitafungua dimba hiyo kesho kwa mchezo pekee.
Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, imekumbusha vilabu kuzingatia, Kanuni ya 42 (27) ya Ligi Kuu inayosema: “Klabu ambayo haitapeleka uwanjani timu ya U-20 mechi ya kwanza itapigwa faini ya Sh 2,000,000 na kunyang’anywa na kupoteza mchezo, mechi ya pili itapigwa faini ya Sh 2,000,000 na kunyang’anywa pointi tatu katika Ligi ya Wakubwa (Ligi Kuu) na Ligi ya Wadogo (U-20).