Thursday , 17th Nov , 2016

Ligi Kuu ya Soka ya wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena Novemba 20 baada ya kusimama kupisha mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars na timu ya Taifa ya Cameroon.

 

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, ligi hiyo itachezwa mpaka mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu ambapo itaenda kwa mapumziko kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili.

Lucas amesema, ligi hiyo itamaliza mzunguko wa kwanza mwishoni mwa Desemba kutokana na kupelekwa mbele kwa ratiba mara baada ya timu ya taifa kuwa katika maandalizi ya mechi dhidi ya Cameroon.

Amesema, ligi hiyo bado inahitaji sapoti ya wadau mbalimbali wa soka hapa nchini ili kuweza kufikia katika malengo ikiwa ni pamoja na kuweza kupata zawadi kwa bingwa wa michuano hiyo pamoja na kupata vipaji bora zaidi ambavyo vitaisaidia pia timu ya taifa.