Thursday , 29th Oct , 2015

Baada ya kusimama kwa muda wa wiki mbili kupisha uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu, Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD kesho kinaendelea na ratiba zake za michuano ya ligi ya mkoa RBA.

Ligi hiyo iliyopo kwenye mzunguko wa kwanza tangu ilipoanza kuunguruma Oktoba nne mwaka huu inazishirikisha jumla ya klabu 18 za wanaume na wanawake za jijini Dar es salaam.

Katika michezo miwili ya kesho timu ya wanaume ya maafande wa JKT inatarajia kukutana na Chui, ukiwa ni mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo na katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa ndani wa Taifa, Chui ilichapwa kwa point 100-75.

Wakati mchezo mwingine wa kesho utakuwa kati ya Savio na Vijana