Saturday , 5th Apr , 2014

Michuano ya klabu bingwa ya taifa ya mpira wa kikapu imeanza hii leo katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam na inataraji kuhitimishwa April 12 mwaka huu

Moja kati ya michezo ya Kikapu iliyofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa

Michuano ya klabu bingwa ya taifa ya mpira wa kikapu imeanza hii leo katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam na inataraji kuhitimishwa April 12 mwaka huu.
Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF Saleh Zonga amesema kuwa michano ya mwaka huu imeweka rekodi ya aina yake msimu huu kwa timu nyingi kujitokeza hasa za mikoani ambapo timu ambazo zimefika katika michuano hiyo ni 26,wanaume vilabu 22 na wanawake vilabu 4.
Aidha Zonga amesema anategemea michuano itakwenda vizuri pamoja na kukosa udhamini.
Katika Tennis michuano ya vijana chini ya miaka 10 na 12 imeanza hii leo katika viwanja vya klabu ya Dar Gymkhana ikishirikisha wachezaji zaidi ya 50 wakichuana kutafuta pointi zitakazowawezesha kufuzu katika nafasi nzuri katika michuano mikubwa ya vijana.
Mratibu wa michuano hiyo ambaye ni mjumbe wa kamati ya ufundi ya chama cha Tennis Tanzania TTA Fouard Somi amesema uwepo wa vijana wengi waliojitokeza safari hii kumeongeza msisimko na ushindani na hivyo kuinua mwamko wa michuano hiyo.