Sunday , 13th Mar , 2016

Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea tena leo hii kwa kupigwa michezo minne ambapo Simba inawakaribisha wajelajela Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba inavaana na Prisons ikiwa inajivunia pointi 51 zinazomuweka kileleni huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya tano kwa Pointi 36.

Wanalizombe Majimaji ya Songea mkoani Ruvuma watakuwa katika dimba la Majimaji kuwaalika Stand United ya Shinyanga huku wanankurukumbi Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga.

Dimba la Kambarage mkoani Shinyanga, wanajeshi wa Mgambo JKT watawaalika Mwadui CCM Mkwakwani mjini Tanga.