
Kocha wa timu ya vijana Bakary Shime amesema, nguvu zinazowekwa kwenye michezo mashuleni zingewekwa katika kuendeleza michezo kwa ujumla nchi ingekuwa mbali sana na kama ingesimamishwa ndipo ingekuwa na athari kubwa.
Shime amesema, Serikali imezuia mashindano fainali za mashindano ya mashule na sio michezo mashuleni kwani ilishafanyika na hatua ya fainali ilikuwa ni kuhitimisha tuu na hata kusimamishwa kwa michezo ni kwasababu maalumu ambayo ni utengenezaji wa madawati ambao ni muhimu kwa wanafunzo pia.
Shime amesema, watanzania wasipige kelele kwenye michezo mashuleni bali wapige kelele kwenye vyama vya michezo vya mikoa na wilaya ambapo ndipo sehemu vipaji vya watoto vinapotokea.
Shime amesema, shule zinazofundisha michezo ni chache na watoto wanaoshiriki michezo ya mashuleni wanafundishwa katika vilabu vyao vya mitaani na wanachezea shule zao kwa sababu ni wanafunzi lakini hawafundishwi michezo mashuleni.