Tuesday , 7th Jun , 2016

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm amelazimika kukatisha mapumziko yake nchini Ghana, kwa ajili kuwahi kuja kujiandaa timu kwa ajili ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), linaloanza wiki ijayo.

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm.

Pluijm amesema kwamba michuano hiyo ni migumu na hawapaswi kufanya mazoezi ya zimamoto hivyo nilazima kujipanga vizuri kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kucheza fainali.

“Mechi za Kombe la Shirikisho zina ugumu, ninahitaji kuanza maandalizi mapema zaidi ili kuwa fiti kwa ajili ya kutimiza malengo yetu tuliyojipangia msimu huu,” amesema Pluijm.

Yanga imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwatoa Sagrada Esperanca ya Angola.