
Kocha wa Simba Patrick Aussems.
Aussems ameyasema hayo leo kwenye mkutano na wanahabari mjini Kitwe, Zambia ambapo amesisitiza umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu unaufanya uwe na asilimia 50 kwa 50 hivyo ni muhimu kuwa makini.
''Ninafahamu Nkana ni timu nzuri lakini na sisi ni timu bora na tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo yakayotubeba kwenye mchezo wa pili jijini Dar es salaam'', amesema Aussems.
Kwa upande wa mchezaji, Haruna Niyonzima ambaye ameongea kwa niaba ya nahodha John Bocco, amesema wao kama wachezaji wameshapokea kile walichofundishwa na mwalimu na wameahidi kutekeleza uwanjani.
Mchezo huo wa kwanza katika raundi ya kwanza ya klabu bingwa Afrika, unapigwa kesho Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni.