Akifanya mahojiano na mtandao wa timu hiyo, Pierre ameweka wazi kuwa katika mpango wake wa miaka mitano anatarajia kuanzisha timu imara za vijana chini miaka 17, 20 na 21.
Kocha huyo ambaye mkataba wake haujawekwa wazi kuwa ni wa muda gani ameeleza kiu yake kuwa ni kuona timu hizo za vijana zinacheza mfumo sawa na timu ya wakubwa na hiyo itarahisisha timu kuwa na mfumo wake utakaoipa mafanikio.

''Timu za vijana tutakazozianzisha kama ni ya miaka 17 wacheze sawa na vijana wa miaka 20 na 21 na wakipanda katika timu ya wakubwa iwe rahisi tu kucheza mfumo huo ambao ndio utaipa Simba mafanikio'', amesema.
Pierre Lechantre alianza kukaa kwenye benchi la ufundi la Simba SC kama kocha mkuu kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Majimaji FC, mchezo uliopigwa jumapili iliyopita uwanja wa taifa Dar es salaam.
