Saturday , 6th Feb , 2016

Shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF, wako kwenye mchakato wa mwisho kusaini mkataba wa miaka miwili na kocha wa kigeni kutoka nchini Marekani, kwaajili ya kuja kuifundisha timu ya taifa ya mchezo huo.

Rais wa shirikisho hilo la mpira wa kikapu nchini, Eng. John Bandiye, amesemakuwa kocha huyo aliyemtaja kwa jina moja la Mathew, aliwahi kuja nchini kwa majaribio mwishoni mwa mwaka jana, na atasaidia pia kufundisha timu ya watoto, na kwamba pamoja na mambo mengine,ameahidi misaada mbalimbali kutoka nchini Marekani kwaajili ya kukuza mchezo huo hapa nchini.

Hivi karibuni serikali ilitangaza vyama vya michezo kuhakikisha vinajipanga kuanza kuwagharamia walimu wake, tofauti na awali ambapo serikali chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ilichukua jukumu hilo kwa kutenga mafungu ya kuwalipa walimu wa timu za taifa za michezo mbalimbali.