Thursday , 23rd Jul , 2015

Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kombe la Kagame inaingia katika siku yake ya saba kesho ambapo KMKM ikimalizia mchezo wake wa mwisho kwa kuumana na mabingwa wa ligi kuu Soka Tanzania Bara, Young Africans uwanja wa Taifa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, afisa habari wa Shirikisho la soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, mchezo huo utatanguliwa na vinara wa kundi A timu ya Gor Mahia ikimenyana na Khartoum uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kizuguto amesema, iwapo KMKM itapoteza mchezo dhidi ya Yanga itakuwa imejiondoa katika michuano hiyo na kama Yanga ikipoteza itakuwa imejiweka katika hatari ya kujiondoa kwani itakuwa imebakiza mchezo mmoja katika hatua ya mzunguko.