Akiongea kuelekea mchezo wa EPL kati ya timu yake ya Liverpool dhidi ya Tottenham Klopp amekiri hilo kwa kudai haoni nafasi kwa timu zingine kwasababu Manchester City haioneshi dalili za kukwama.
“Manchester City inafanya vizuri na nafikiri wananafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa kuliko timu zingine japokuwa kwenye soka lolote linawezekana amesema”, amesema Klopp
Liverpool ambayo ina pointi 13 katika nafasi ya 8 imekuwa haina mwendelezo mzuri kwenye ligi japokuwa Klopp ana imani na timu yake kuwa inaweza kufanya vizuri.
Endapo Liverpool itashinda leo dhidi ya Tottenham itafikisha alama 18 na kupunguza tofauti ya alama dhidi ya vinara Manchester City wenye alama 25.