
Kilimanjaro Stars ilijipatia bao lake la kwanza ndani ya dakika ya 23 kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Kiungo Said Ndemla ambalo lilidumu mpaka dakika 45 za kwanza ambapo timu zikwenda mapumziko matokeo yakiwa ni 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana huku Rwanda ikionesha dalili za kuhitaji kusawazisha lakini bahati haikuwa upande wao na katika dakika ya 77 Kilimanjaro Stars iliyo chini ya kocha Abdallah Kibaden ilijipatia bao la pili lililotiwa nyavuni na mshambuliaji Simon Msuva baada ya Mlinda Mlango wa Rwanda kuacha goli.
Katika dakika ya 89 Jacques Tuyisenge aliipatia Rwanda bao la kufutia machozi ambapo kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars imejihakikishia kuingia hatua ya Robo fainali ambapo mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi itakutana na mwenyeji Ethiopia siku ya Alhamisi.