
Kilimanjaro Qeens
Kilimanjaro Queens na Burundi zinatarajia kutumia mchezo huo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Chalenji kwa wanawake yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 11 mpaka 20 mwaka huu mjini Jinja, Uganda.
Kocha wa Kilimanjaro Queend Sebastina Mkoma amesema, mechi hiyo itamsaidia kuimarisha kikosi chake na kuangalia upungufu kabla ya kwenda kwenye michuano hiyo.
Mkoma amesema, wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wanatarajia wapinzani wao Burundi watawapa mazoezi yanayostahili kuelekea katika kuwania kombe hilo.
Kilimanjaro Queens imepangwa kundi B ikiwa na Ethiopia na Rwanda wakati kundi A likiwa na timu mwenyeji Uganda, Zanzibar, Burundi na Kenya.