Wednesday , 25th Jan , 2017

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amefunguka na kusema kuwa sasa kikosi cha Yanga kimekamilika kwani wachezaji wote ambao walikuwa majeruhi wameanza mazoezi na hali zao ziko vizuri.

Makocha wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu

Juma Mwambusi ameyasema hayo katika mazoezi ya kikosi chake na kusema kuwa hali za wachezaji ziko vizuri na wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa siku ya Jumapili.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani mahudhurio yamekuwa mazuri wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea na tayari wameanza kufanya mazoezi ya pamoja na kikosi kuelekea mchezo wa Jumapili ambao ni muhimu sana kwetu kupata point tatu mbele ya wapinzani wetu Mwadui Fc" alisema Mwambusi

Mbali na hilo kocha huyo msaidizi alisema kuwa mchezaji Donald Ngoma yeye bado hajarejea nchini, yuko Zimbabwe kutokana na matatizo ya msiba wa kaka yake ambao ulitokea nchini humo.