
Kamishna wa ufundi wa mashindano wa chama cha mpira wa kikapu nchini TBF Manase Zabron amesema, mashindano hayo yalitakiwa kufanyika Oktoba mwaka jana lakini walikuwa hawajapata mdhamini wa mashindano hayo.
Kwa upande mwingine Manase amesema, mashindano ya kanda ya tano ya mpira wa kikapu yaliyokuwa yafanyike Julai mwaka huu yamepelekwa mbele mpaka Octoba mwaka huu kutokana na mashindano ya majeshi ya Afrika Mashariki na kati yanayofanyika Kigali nchini Rwanda.
Manase amesema, mashindano hayo yanashirikisha timu mbalimbali za jeshi ambazo pia zingetakiwa kushiriki mashindano ya kanda ya tano.
Manase amesema, wanasubiri mpaka mashindano hayo yatakapomalizika na baada ya hapo wanaendelea na maandalizi ya kanda ya tano.