Friday , 11th Nov , 2016

Kifo cha mwanamichezo, Hafidh Ali Tahir, kimeacha majonzi makubwa huku wabunge ambao ni wanasoka wakimlilia na kusema mchango wake katika sekta ya michezo bungeni hautasahaulika.

Marehemu Hafidh Ali Tahir

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wabunge hao wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda, amesema marehemu Hafidh alikuwa kocha mzuri katika michezo.

Awali akisoma wasifu wa marehemu kwa upande wa soka, mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu, amesema wabunge wamepata pengo kubwa kwa kuondoka kwake.

Hafidh amekuwa mbunge wa Dimani na amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikoenda kupata matibabu kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu.

Wasikize hapa wakimzungumzia.........

Sauti ya Sixtus Mapunda
Sauti ya Musa Azan 'Zungu'