Wednesday , 8th Mar , 2017

Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya mapokezi makubwa ya kifimbo cha malkia ambacho kinatarajiwa kutua nchini mwanzoni mwa mwezi ujao na kutembezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Arusha.

Wanamichezo Filbert Bayi (kushoto) wa Tanzania, Kipchoge Keino wa Kenya, wakiwa wameshikilia kifimbo cha Malkia.

 

Taarifa ya ujio wa kifimbo hicho imetolewa hii leo na uongozi wa kamati ya Olimpiki Tanzania TOC ambapo Rais wake Gulam Rashid amesema ujio wa kifimbo hicho ni kuwaka kwa taa ya kijani ya kuashiria kuanza michuano ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika mwakani nchini Australia.

Kwa upande wake katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amesema mbio za mwaka huu katika kukimbiza kifimbo hicho zitakuwa na mabadiliko hasa katika idadi ya wale watakaoshika kifimbo hicho moja kwa moja.