Thursday , 24th Nov , 2016

Kevin Love ameweka rekodi mpya kwenye NBA kwa kufunga pointi 34 kwenye robo ya kwanza na kusaidia Cleveland Cavaliers kushinda vikapu 137-125 dhidi ya Portland Trailblazers.

Kevin Love

 

Love mwenye umri wa miaka 28, alifunga three-pointers nane, na kujiwekea rekodi hiyo, kama mchezaji kwenye robo moja ya Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani, NBA.

Love anaweka rekodi hiyo, wakati tayari mapema mwezi huu, Stephen Curry wa Golden State Warriors akiweka rekodi ya kufunga three-pointers 13 kwenye mchezo mmoja.