Nyota mpya wa Golden State Warriors Kevin Durant(pichani) akiwa katika jezi za Oklahoma City Thunder.
Durant mwenye umri wa miaka ishirini na saba ameyasema hayo wakati akithibitisha kuondoka kwake OKC na kusaini mkataba wa miaka miwili na Golden State Warriors unaoripotiwa kuwa na thamani ya dola milioni hamsini na nne.
Akizungumza mara baada ya taarifa hiyo Durrant amesema ni muda muafaka kwake kujaribu kuboresha mchezo wake katika timu nyingine huku wachambuzi wa mambo wakitaja uhamisho huo ni kutokana na kiu ya nyota huyo kusaka ubingwa wa NBA.
Nyota huyo ambaye amejumuishwa katika kikosi cha USA kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki mwaka huu anakwenda kuungana na wakali wengine kama Steph Curry na Klay Thompson ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika timu hiyo.
Kuwasili kwa Durant ndani ya Golden State Warriors kuziba mapengo yaliyoachwa na Andry Bogat na Harrison Barner waliotimkia Dallas Mavarecks.


