Mabondia wa ngumi za ridhaa wakichuana katika moja ya michuano ya Temeke.
Chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Temeke TEABA kimesema bado kinaendelea na maandalizi ya michuano ya kimataifa ya ngumi itakayofanyika mkoani humo kuanzia mwanzoni mwa mwezi September mwaka huu japo chama hicho kinakabiliwa na ukata
Mwenyekiti wa TEABA Said Omar Gogo Poa amesema kiutawala wanaendelea na maandalizi kama kawaida japo wanakabiliwa na ukata katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa mafaniko makubwa na kuwezesha kukuza vipaji vya vijana ambao ndio walengwa wa michuano hiyo
Aidha Gogo poa amesema tayari wakenya ambao ni miongoni mwa nchi 3 waalikwa wakiwa sambamba na nchi za Uganda na Zambia wamethibitisha kuleta vilabu vitatu vya ngumi na hivyo amewataka mabondia wa Tanzania kufanya maandalizi ya kutosha ili kubakiza ushindi nyumbani kwani itakuwa ni aibu kwa Tanzania kama wenyeji kuacha wageni wakiondoka na medali
Gogo poa amewaomba wadau,makampuni na wadhamini mbalimbali kujitokeza kusaidia kwa hali na mali ili kufanikisha mashindano hayo kwani yana hadhi ya kimataifa ili yaweze kufanyika kwa mafanikio makubwa.