Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kufunga goli katika moja ya michezo ya ligi kuu.
Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imesema mchakato wa kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi za Uongozi katika klabu hiyo unaendelea vizuri baada ya kamati hiyo kukutana hapo jana na kinachosubiriwa hivi sasa ni Katiba ya kbabu hiyo iliyopelekwa kusajiliwa kwa Msajili mara baada ya marekebisho kadhaa.
Akiongea jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Klabu hiyo,Dakta Damas Ndumbaro amesema mara baada ya Katiba hiyo kukabidhiwa klabu ya Simba waanza mara moja mchakato wa Uchaguzi huku akiiomba Ofisi ya Msajili kuharakisha mchakato wa kuisajioli katiba hiyo.
Ndumbaro amesema katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho madogo katika klabu hiyo na kupitiwa na shirikisho la soka nchini Tanzania katika baadhi ya vipengele hivyo usajili rasmi ni muhimu ili kutangaza tarehe rasmi ya kuanza kutolewa fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika klabu hiyo.