
Katika taarifa yake kutoka nchini Afrika Kusini Ngassa amesema Kamati zilizoundwa zinapaswa kufanya shughuli zake vizuri na kwa umakini ili malengo yatimie.
Tanzania itacheza mara mbili na Algeria ndani ya siku tatu nyumbani na ugenini kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.