Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema, wote wenye matatizo watafikishwa mbele ya kamati na kuchukuliwa hatua kutokana na kila kosa alilotenda ili iwe fundisho kwa wengine.
Wambura amesema, kila klabu inajua kanuni na sheria za mpira hivyo vurugu zinazosababishwa na timu pamoja na mashabiki ni wazi kwamba wanafanya huku wakiwa wanajua kuwa haitakiwi na kuna adhabu ambazo zipo kutokana na makosa watakayoyafanya.
Wambura amesema, anaamini kamati ya sheria itatoa hukumu ili kuweza kulinda hadhi na kupata wadhamini katika soka kwani kama vurugu zikiendelea hamna mdhamini atakayeweza kujitokeza kwa ajili ya kusaidia soka nchini.





