Tuesday , 23rd Jan , 2018

Kocha mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba leo ameongelea mchezo wao wa ligi ujao dhidi ya mabingwa watetezi Yanga utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Azam Complex.

Cioaba amesema mchezo huo utakuwa mgumu na watacheza kwa umakini ili waibuke na ushindi. 

“Hautakuwa mchezo mwepesi nitakuwa na muda wa siku tatu wa maandalizi kwa kuwa nina safari ndefu sana na wachezaji wanauchovu kidogo lakini nitatumia siku hizo kuunganisha vyema wachezaji na kujaribu kufanya vizuri katika mchezo huo'', amesema.

Cioaba ameongeza kuwa anaiheshimu Yanga kwasababu   ni moja ya timu kubwa nchini na ndio mabaingwa watetezi wa ligi hivyo hategemei kama watapata urahisi.

Katika mechi 14 za ligi, Azam FC haijapoteza mchezo na  imeshinda mechi nane na kutoa sare sita ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 30 ikizidiwa na Simba yenye alama 32.