
Moja ya mechi ya kombe la shirikisho iliyopigwa jijini Dar es salaam
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja ambapo Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Ilulu – Lindi.
Disemba 24 Njombe Mji watakuwa wenyeji wa Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.
Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisams Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.
Mzunguko huo wa pili unatarajiwa kumalizika Desemba 29 mwaka huu kwa michezo minne ambayo ni
Wenda FC v Kimondo (Sokoine),
Mji Mkuu (CDA) v Singida United (Jamhuri),
Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika),
Abajalo FC v Villa Squad (Karume).
Timu saba za Ashanti United, Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.