
Ambapo kocha mkuu wa timu hiyo ya maafande wa jeshi la kujenga taifa Mary Frank amejinasibu kulibakisha kombe hilo hapa nchini kutokana na mazoezi waliyofanya kwa takribani mwezi mmoja huku pia sapoti ya uongozi wa jeshi ukichagiza na kuongeza morali ya timu
Naye nahodha wa timu hiyo Mwanaidi Hassan amesema kikosi chake kiko tayari kufanya maajabu kama waliyofanya katika michuano ya mwaka 2009 kwa kutwaa ubingwa huo,
Mwanaidi amesema kuwa pamoja na kumkosa mwenzao mmoja lakini wachezaji waliobaki wako katika morali ya juu na pengo hilo halitaonekana.
