Friday , 28th Mar , 2014

Timu ya wanawake ya JKT Mbweni ya Tanzania imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya netiboli ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuifunga timu ngumu ya Prisons ya Uganda wa magoli 35-33, katika mchezo ambao ulichelewa kuanza kutoka na

Mechi hiyo ni moja kati ya nusu fainali mbili za michuao hiyo ambayo imepigwa hii leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam

Mechi hiyo ilichezwa sambamba na nusu fainali nyingine kati ya NIC ya Uganda na MOIC ya Kenya ambapo NIC imeshinda kwa magoli 49-32 na hivyo itakutana na JKT Mbweni katika fainali itakayopigwa hapo kesho uwanja wa taifa

Na mara baada ya mchezo kati ya JKT mbweni ya Tanzania na Prisons ya Uganda muhtasari wa michezo umezungumza na kocha Mary Frank na nahodha wa timu ya JKT Mbweni ya Tanzania Mwanaidi Mohamed wanazungumziaje ushindi huo kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya NIC ya Uganda

Kwa upande wake kocha mkuu wa timu ya Prison ya Uganda Nyongesa Imelda amesema amepokea matokeo hayo kwani ni sehemu ya mchezo lakini akisikitishwa na wachezaji wake kutofuata maelekezo yake na kusababisha JKT Mbweni kurejea mchezo katika robo ya pili ya tatu na ya nne baada ya wao kuongoza katika robo ya kwanza na hivyo kutolewa katika hatua hiyo ya nusu fainali.