Tuesday , 9th Jun , 2015

Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Jabir Aziz Stima amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu ya MwaduI FC.

Katika taarifa yake, Stima amesema, anaamini kusaini kwake Mwadui kutazidi kumfungulia zaidi milango ya kuendelea kusonga mbele katika soka hapa nchini.

Stima amesema, maisha ya soka kwa mchezaji ni popote na anaamini ataweza kuifanyia mazuri klabu hiyo ambayo imepanda kucheza ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao.

Kabla ya kusaini Mwadui, Stima alikuwa akikipiga JKT Ruvu ambayo nayo ilimsajili baada ya kutemwa Azam FC.