Monday , 7th Apr , 2014

Hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu NBL imeendelea hii leo katika uwanja wa ndani wa taifa huku Ilala ikikacha mchezo wao dhidi ya Vijana city bulls ya kinondoni

Timu ya mpira wa kikabu ya vijana ya Dar es salaam imepata ushindi wa chee baada ya timu ya Ilala kuingia mitini katika mchezo wa hatua ya makundi katika michuano ya klabu bingwa ya taifa ya mpira wa kikapu inayoendelea katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na EATV Msimamizi wa Waamuzi katika michuano hiyo, Haleluya Kavarambi amesema Kufuatia timu ya Ilala kuingia mitini bila kutoa taarifa yoyote, timu ya vijana imepewa Work-Over yaani pointi mbili na magoli ishirini hatua hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa kanuni za mchezo wa mpira wa kikapu.

Akimalizia Kavarambi amesema kama timu itakosa michezo mitatu bila kutoa sababu yoyote ya kimsingi basi kwa mujibu wa kanuni itakua imejiondoa moja kwa moja katika michuano hiyo na hivyo matokeo ya michezo yote iliyokwishacheza yanafutwa.