Monday , 15th May , 2017

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara amedai anaonewa kwa kupewa lawama zisizomuhusu baada ya kile kinachoaminiwa kuwa naye ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika makubaliano na mdhamini wao mpya Sportpesa

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara

Manara amesema hayo siku moja baada ya mfanyabiashara , Mohammed Dewji kutoa kauli ya kusikitishwa na uongozi wa klabu ya Simba kusaini mkataba wa udhamini wa muda mrefu na Sportpesa bila ya kumshirikisha yeye, ambaye aliweka nguvu zake nyingi katika klabu hiyo.

"Uongozi wowote ni Jalala ila uongozi wa mpira ni Dampo, 'sometimes' napokea lawama zisizonihusu, 'but' nina moyo wa chuma na nina uzoefu wa kuwa kiongozi katika tasnia tofauti, kazi yangu ni kuhabarisha umma, mengine ni kunionea". Aliandika Manara kupitia ukurasa wake wa instagram