Thursday , 14th Jan , 2016

Bingwa wa zamani ngumi duniani Muingereza David Haye, ameahidi kurejesha heshima yake katika mchezo huo duniani kwa kumtwanga Mark De Mori siku ya Jumamosi wiki hii.

Bingwa wa zamani ngumi duniani Muingereza David Haye, ameahidi kurejesha heshima yake katika mchezo huo duniani kwa kumtwanga Mark De Mori siku ya Jumamosi wiki hii.

Haye mwenye umri wa miaka 35, amedai kuwa, hili ndilo pambano pekee ambalo linaweza kumrejeshea heshima kwa mara nyingine, hivyo anajiami kuwa ushindi kwake ni lazima.

Ameongeza kuwa asingeweza kukubali kucheza pambano ambalo anajua kuwa atapoteza, na kama ikiwa hivyo basi ni bora kwake kustaafu mchezo huo hata kama atashinda.

Haye alishinda mkanda wa WBA uzito wa juu mwaka 2009 na kuupoteza miaka miwili baadaye kwa kupigwa na Wladimir Klitschko wa Ukraine huku akitangaza kustaafu mwaka 2013 baada ya kupata majeraha ya bega.

Pambano lake la mwisho alimpiga Dereck Chisora mwaka 2012 na sasa anapambana kurejesha heshima kupitia kwa Mark De Mori kutoka Australia siku ya Jumamosi hii.