Wachezaji wa Yanga
Yanga ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa, itashuka dimbani kucheza na Alliance Jumamosi hii katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
"Utakuwa mchezo mgumu na ni muhimu kwetu kupata pointi tatu tunataka kushinda sio tukicheza Dar tu bali tumejiandaa kushinda hadi mikoani, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kutamba katika ligi na atuna presha yoyote kuhusu mchezo huo", amesema.
Aidha Kaya amewaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu yao kwa kuingia uwanjani siku ya mchezo huo kwani wao ni wachezaji wa 12 ambao huwapa nguvu wachezaji ya kutafuta matokeo mazuri.
Msimu huu, Yanga haijapoteza mechi yoyote katika mechi sita ilizocheza. Imeshinda tano na sare moja, huku ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 16.
Alliance yenyewe imecheza mechi 9, imeshinda moja, sare 3 na kupoteza 5. Inashika nafasi ya pili kutoka chini ikiwa na pointi sita.


