Tuesday , 19th Jan , 2016

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho na keshokutwa, huku macho ya mashabiki yakiwa kwa miamba watatu wanaofukuzana kileleni, Azam FC, Simba na Yanga SC.

Yanga SC inaongoza ligi kuu kwa wastani wa mabao, ikiwa inalingana kwa pointi (36) na Azam FC iliyo nafasi ya pili, wakati Simba SC inafuatia ikiwa na pointi 30.

Akizungumza na East africa Radio, Kocha Msaidizi wa JKT Ruvu Mrage Kabange amesema, wameweka pembeni matokeo yaliyopita dhidi ya Mgambo ambapo walipigwa bao 5-1 ambapo hivi sasa wanaangalia mechi iliyo mbele yao dhidi ya Simba SC.

Kabange amesema, wamepanga kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo japo watanzania wana fikra tofauti ya kuwa JKT Ruvu huwa wanazipania timu za Simba na Yanga jambo ambalo sio la kweli.

Kabange amesema, Simba na Yanga zote zipo sawa na timu zilizopo ligi kuu na wanaamini kucheza Simba au Yanga ni mchezo rahisi zaidi kuliko kucheza na timu mbazo zipo chini.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Simba SC watawakaribisha JKT Ruvu ambapo Azam FC watakuwa ugenini uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakiumana na African Sports huku Wajelajela Tanzania Prisons wakiwakaribisha Coastal uwanja wa Sokoine jijini mbveya.

Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Stand United watawakaribisha Toto African ya jijini Mwanza huku Ndanda wakiumana na Mbeya City uwanja wa Nanganda sijaona Mtwara.

Mzunguko huo wa 15 unatarajiwa kukamilika Alhamisi ambapo uwanja wa Taifa Yanga wataikaribisha Majimaji huku Mwadui akiikaribisha Kagera Sugar uwanja wa Mwadui.