Bingwa mara mbili mfululizo wa Formula One Lewis Hamilton (pichani) katika moja ya mbio za mashindano hayo.
Hamilton amemaliza katika nafasi ya tano kwenye mashindano ya European Grand Prix na kumfanya awe nyuma kwa alama 24 dhidi ya dereva mwenzake wa Mercedes Nico Roseberg ambaye ametamba kwenye mbio hizo.
Akizungumza mara baada ya mashindano kumalizika Muingereza huyo amesema kuwa huu ni mwaka mzuri kwa Nico lakini bado hajakata tamaa kwa kuwa bado ana nafaisi ya kufanya vizuri katika mashindano yaliyosalia.
Bingwa huyo wa dunia mara mbili mfululizo alipunguza tofauti ya alama kutoka 43 hadi kufikia tisa dhidi ya Nico baada ya kushinda mara mbili mfululizo lakini amekutana na kikwazo hapo jana kutokana na injini yake kupata hitilafu wakati wa mashindano.


