Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa TAVA Mwarame Mchume amesema, mpaka sasa FIVB limeshatuma jina la mkufunzi kutoka nchini Ethiopia anayefahamika kwa jina la Tsefaye anakayefundisha jinsi ya kuendesha mchezo wa mpira wa wavu na jinsi kuutumia kupata wafadhli ili kuzipa wigo mpana timu kuweza kupata fursa ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Mchume amesema, baada ya kozi hiyo, TAVA itaendelea kusimamia mikoa ili kuhakikisha inaendesha Ligi kikamilifu ili kuweza kupata timu bora zitakazoshiriki mashindano ya Taifa.


