Thursday , 1st May , 2014

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Nicholas Meignot hii leo amefungua semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mwenyekiti wa CECAFA, Leodgar Tenga

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Nicholas Meignot hii leo amefungua semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Maignot katika mkutano huo wa siku mbili unaofanyika jijini Dar es Salaam amefuatana na maofisa wengine saba wa FIFA ambapo amesema lengo la semina hiyo ni kuhakikisha wanautangaza mchezo wa soka duniani kote

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Leodger Tenga ameishukuru FIFA kwa kutoa fursa hiyo kwa CECAFA na akatoa wito kwa viongozi wote kutoka nchi 12 wanachama wa CECAFA waliohudhuria semina hiyo kuhakikisha wanaitumia vema nafasi hiyo