Tuesday , 7th Jun , 2016

Daktari wa zamani wa Chelsea, Eva Carneiro, anatarajiwa kuielezea mahakama ya kazi, jinsi kocha wa zamani wa klabu hiyo Jose Mourinho alivyokuwa akimnyanyasa kijinsia na kumdharau katika kazi ya ndoto zake.

Daktari wa zamani wa Chelsea, Eva Carneiro.

Ikiwa ni siku 300 na 4, baada ya mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu uliomalizika, kwenye uwanja wa Stamford Bridge, mechi kati ya Chelsea na Swansea, Daktari Carneiro atasimama huko Croydon, London kusini, kutoa ushahidi jinsi alivyonyanyaswa na Kocha Mourihno, licha kufanya vizuri kazi zake, akifuata sheria za mchezo na ufanisi wa kazi.

Kocha Jose Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa Manchester United, anatarajiwa kusimama kwenye Mahakama hiyo ya kazi na kutoa utetezi wake jumatatu na jumanne ya juma lijalo.