
Waamuzi kutoka TBF Gozbert Boniface na Prosper Mushi wakiendesha droo ya mechi za mtoano.
Katika droo hiyo jumla ya timu 50 zimepangwa kuchuana ili kuwatafuta washindi 15, ambao wataungana na bingwa mtetezi kwaajili ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya pili.
Droo hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za East Africa Television, iliongozwa na Kamishna wa Ufundi na Mipango wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manase Zablon pamoja na wawakilishi wa timu hizo 50.
Wawakilishi wa timu shiriki wakifuatilia kwa umakini droo ya mechi ya mtoano.
Kabla ya droo kufanyika timu zote zilisomewa Sheria na kanuni za mashindano kwa msimu huu ambapo wote kwa pamoja walikubaliana na sheria hizo. Moja ya sheria hizo ni timu inaruhusiwa kuwachezesha kwa pamoja wachezaji wawili tu wa daraja la kwanza.
Mechi za hatua ya mtoano zitaanza kutimua vumbi kuanzia Juni 30, 2018. Mechi hizo ni kama zinavyoonekana hapo chini.
1. | Dream Chaser | Vs | TMK Heroes |
2. | The Fighter | Vs | Force One |
3. | Flying Dribblers | Vs | Kurasini Worriors |
4. | TMT | Vs | Street Ballers |
5. | GWU | Vs | External Heroes |
6. | DMI | Vs | Madale State |
7. | Ardhi University | Vs | The Kazi 8 Lycans |
8. | Ukonga Worriors | Vs | Little Saint |
9. | Oysterbay | Vs | Ilala Easzone |
10. | BTP | Vs | Grounders |
11. | Oratory | Vs | Mbezi Beach KKKT |
12. | The Sniper | Vs | Young Boys |
13. | Eagle Wings | Vs | Portland |
14. | Golden Talent | Vs | Montefort Kings |
15. | Ukonga Hitmen | Vs | Yombo Patroit |
16. | The Hashtag | Vs | BV |
17. | Bankers | Vs | Water Insititute |
18. | NIT Ballers | Vs | Air Wings |
19. | Fast Heat | Vs | Street Worriors |
20. | Stylers | Vs | Denth Shoppers |
21. | Loyo Light | Vs | Kigamboni City |
22. | K-Worriors | Vs | Team Kiza |
23. | Madena | Vs | St. Joseph |
24. | The Magic | Vs | Raptors |
25. | Weusi | Vs | Kichangani |