Sunday , 23rd Dec , 2018

Baada ya ushindi wa Simba wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana FC, msemaji wa wapinzani wa Simba nchini klabu ya Yanga Dismas Ten ameipongeza Simba kwa ushindi huo.

Kushoto ni Dismas Ten na kulia ni Clatous Chama.

Muda mchache baada ya mechi kumalizika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Dismas ameweka ujumbe wa pongezi kwa kuanika ''Hongereni sana....!'', ameandika.

Ushindi huo wa Simba umeifanya timu hiyo kuwa wawakilishi pekee wa Tanzania ambao wamefika hatua ya makundi klabu bingwa Afrika katika miaka 20 iliyopita.

Misimu miwili iliyopita Yanga ilitinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika lakini haikufanikiwa kuvuka hatua hiyo.