Monday , 30th Jan , 2017

Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za bongo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza

Marehemu David Burhan

Taarifa za awali zinasema kuwa Burhan alikuwa akisumbuliwa na homa ya manjano wakiwa safarini na timu, lakini timu iliporejea Kagera hali ikawa mbaya na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando.

Taratibu za mazishi zinafanywa na mipango ikikamilika, anaweza kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Iringa.

Kwa mujibu wa kaka yake, Marehemu ameacha mke na watoto wawili.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani"

Marehemu David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es Salaam, Abdallah Buruhan.