Thursday , 26th Feb , 2015

Chama cha mchezo wa Vishale (Darts) TADA kimesema, wapo katika mchakato wa kuandaa mashindano ya kutafuta mchezaji mmoja mmoja na wawiliwawili wenye viwango ambayo inatarajia kufanyika Machi mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa TADA, Kale Mgonja amesema michuano hiyo itashirikisha kanda tano ambazo ni kanda hizo ni kanda ya Ziwa, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini na kanda ya Kati ambapo lengo hasa la michuano hiyo ni kuweza kupata vipaji vipya ambavyo vitakuwa kwa vijana.

Mgonja amesema, michuano hiyo itashirikisha watu mbalimbali ambapo sehemu kubwa ikiwa ni wanavyuo huku fainali za michuano hiyo ikitarajiwa kufanyika Mjini Moshi April mwaka huu.